Kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Limited inafanya kazi na watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendeleza visima vya gesi asilia ya Songo Songo takriban kilomita 140 kusini ya Dar es Salaam. Gesi asilia kutoka Kisiwa cha  Songo Songo hutumika kuzalisha umeme  Dar es Salaam na hutumika pia kutoa nishati inayotumiwa na mtambo wa kuzalisha saruji Wazo Hill na viwanda zaidi ya 35 katika eneo la Dar es Salaam.

PanAfrican Energy inajivunia gesi asilia ya Songo Songo na inafanya kazi kwa kushirikiana na makampuni ya Tanzania katika kuendeleza rasilimali za nishati Tanzania.. Wafanyakazi wetu wa Tanzania wanatumia ujuzi na uzoefu walionao kuongeza upatikani wa gesi asilia kama nishati safi ya kuzalisha umeme, kutumika viwandani na kukidhi mahitaji ya Biashara na Usafiri Dar es Salaam.

Kama angependa kufanya majadiliano na sisi katika lugha ya Kiswahili juu ya kampuni yetu na shughuli zake tafadhali wasiliana na ofisi zetu za Dar es Salaam na omba kuzungumza na wafanyakazi wetu katika lugha ya Kiswahili.
Simu: +255 22 2138737